Pages

Pages

Pages

Tuesday, 3 June 2014

MBASHA:NITAJIUA....

Upande wa pili wa shilingi! Kwa mara ya kwanza
tangu ahusishwe na skendo ya ubakaji wa
shemejiye mwenye umri wa miaka 17, mume wa
mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha,
Emmanuel Mbasha ameibuka na kuzungumza na
Uwazi katika mahojiano maalum dhidi ya kashfa
yake hiyo huku akitishia kujiua.


Mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha,akiwa
na mumewe Emmanuel Mbasha.
Akizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa
moja mwishoni mwa wiki iliyopita huku
akikanusha kukimbilia mafichoni baada ya
kuondoka nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar
hivi karibuni, Mbasha ambaye pia ni mwimba
Injili kama mkewe, alianika kila kitu akidai cha
siri kwamba anajua anachezewa mchezo mchafu
baada kuwepo kwa gogoro zito kati yake na
mkewe hadi kutishia uhai wa ndoa yao.

ASIMULIA TUHUMA
“Tuhuma zilizoripotiwa na binti aitwaye...
(anamtaja jina) ambaye kweli ni ndugu wa mke
wangu (Flora) kwenye Kituo cha Polisi Tabata-
Shule (Dar) si za kweli.
“Anayefanya mambo hayo yote ni mke wangu,
anataka nipotee ili awe huru. Mimi najua hilo.”

KASHFA YA KUTENGENEZA
“Hii kashfa ni ya kutengeneza ili nipotee lakini
sipo tayari kupata aibu, bora nijiue.
“Mke wangu amekuwa tatizo kwenye ndoa yetu.
Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha
wakiwa kwenye pozi.
“Kweli ndoa yangu na Flora ina matatizo lakini
matatizo yetu ya ndani sana hakuwa na sababu
ya ‘kuinjinia’ mpango mchafu wa kunimalizia
gerezani mimi ili yeye aponde raha.
“Nyuma ya haya mambo kuna vitu mtu
ukivisema ni aibu sana kwa upande wa pili.
Lakini navijua.”

MKE ALIONDOKA NYUMBANI
“Mke wangu aliondoka nyumbani na kwenda
kuishi hotelini. Hebu fikiria hapo. Mwanzo
alianza kwenda ‘gym’ saa 11:00 alfajiri na kurudi
saa 4:00 asubuhi. Pia saa 10:00 jioni aliondoka
tenda kwenda gym akawa anarudi kati ya saa
3:00 hadi 4:00 usiku.
“Nilipomuuliza alinijibu kuwa ni kwa sababu
anatembea umbali mrefu. Hebu ona sababu ilivyo
dhaifu jamani! Hata kama ungekuwa wewe
mwandishi, unaonaje?”
“Mimi ni mtu maarufu, ningetaka mwanamke
ningepata, iweje nibake?
“Jaribu kufikiria, katika tatizo kubwa kama hili
ambalo linaweza kunifanya nifungwe, nilitarajia
mke wangu awe upande wangu, lakini cha ajabu
yeye ndiye amekuwa nyuma ya adui zangu,
niamini nini mimi zaidi ya yeye kuhusika na
kuniangamiza?”
“Hausigeli wangu ni mzuri, kwa nini nisimbake
yeye?”

AFUATILIA
“Nilipofuatilia niligundua tayari kuna tatizo
kwenye ndoa yetu. Mdudu alikuwa ameingia
ndani ya ndoa kwani hadi sasa mke wangu siishi
naye. Anaishi hotelini.
“Anachokifanya mke wangu ni kitu kibaya mno.
Alimtengeza yule binti ambaye nilikuwa
namsomesha sekondari pale (anataja shule
maarufu Dar), akampa semina ya kutosha
kwamba aseme nimembaka ili nipate
misukosuko na yeye awe huru.
“Kama hiyo haitoshi, akala dili na madaktari,
wakafoji majibu ya vipimo vikionesha kweli yule
binti ameingiliwa, sasa sijui kama vipimo
vilioneshaje kama ni mimi.
“Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia kuona
napandishiwa kizimbani kwa jambo la
kutengenezewa.
“Napiga picha nitakapofikishwa mahakamani jinsi
ambavyo vyombo vya habari vitakavyoandika na
picha zangu kwa kesi ya ubakaji ambayo si ya
kweli.
“Dah! Inaniuma sana. Mke wangu nimemfanyia
vitu vingi sana. Hakustahili kunitendea ubaya
huu. Alikuwa hafahamiani na mtu yeyote
mkubwa. Mimi ndiye nimempeleka kwa watu
wakubwa wakamsaidia sasa amenigeuka,
siamini. Narudia tena, heri kufa kuliko fedheha
hii,” alisema Mbasha kwa uchungu.

HAYUKO MAFICHONI
Kuhusu kuwa mafichoni, Mbasha alisema: “Sipo
mafichoni, sijaambiwa na mtu yeyote nikatoe
maelezo polisi. Nipo nimejaa tele, nikiambiwa
nahitajika nitakwenda kutoa maelezo yangu
kwani sijawahi kutenda kosa hilo na Mungu awe
shahidi yangu.”
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Dar,
Marietha Minangi alithibisha kuwepo kwa ishu
hiyo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.
Flora na Mbasha walifunga ndoa Agosti 22, 2002
hivyo mwaka huu wametimiza miaka 12 wakiwa
pamoja ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa
Elizabeth.

No comments:

Post a Comment