
Linah
akiwa uwanja wa ndege Dar es salaam alipowasili akitokea Johannesburg
South Africa ambako unaweza kwenda Jumatatu Jumatano na Ijumaa kupitia
@fastjet
Katikati ya June 2014 Linah alizungumza na millardayo.com akiwa South
Africa na kuthibitisha kwamba kilichompeleka huko na kumfanya akae kwa
zaidi ya siku 20 ni kazi ya muziki.
Miongoni mwa alivyokua anavifata ni kufanya kolabo na Oskido staa wa
muziki wa Afrika kusini ambae ndio anawasimamia Mafikizolo ambao pia
wanarekodi kwenye studio yake.

Baada ya kutua Dar es salaam akitokea Johannesburg, Linah ameithibitishia
millardayo.com kwamba tayari amefanya kolabo na kundi la Uhuru ambao walishirikishwa kwenye wimbo wa ‘khona’ na Mafikizolo.
Kwenye studio ya Oskido, palepale wanaporekodi mastaa wengine kama
Mafikizolo wenyewe na Davido pia alierekodia hapo kolabo na Mafikizolo,
Linah ndio amerekodi hiyo kolabo na kundi la Uhuru.

Wimbo
wake umefanywa na producer kutoka pia kwenye kundi hilohilo la UHURU
ambae ndio amehusika vilevile kwenye kolabo ya Mafikizolo na Diamond
Platnumz.

Kolabo
alizorekodi South Africa ni mbili ikiwemo moja aliyoshirikishwa na Dj
Malvado ambae yupo kwenye ile hit ya ‘Atchu tchutcha’ ambapo pia Linah
amethibitisha kwamba kwa kipindi chote cha zaidi ya siku 20 Afrika
kusini, amerekodi video na God father Director ambae amefanya video
nyingi kubwa za Afrika zikiwemo za P Square, Davido, Diamond na wengine.
No comments:
Post a Comment