Pages

Pages

Pages

Tuesday, 3 June 2014

KIFO CHA DENT CHUO KIKUU...HUU NDIO UKWELI WAKE.



HATIMAYE  familia ya denti wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, marehemu Sekabenga Pius
Mwakimenya (21) kilichotokea hivi karibuni na
kugubikwa na utata, imeanika ukweli kuhusiana
na tukio hilo.
Akizungumza na Uwazi, mwishoni mwa wiki
iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
baba mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa
jina la Joseph Mwigune alisema, taarifa
waliyopewa na daktari aliyemfanyia uchunguzi
inamaliza utata na minong’ono yote
inayoendelea chuoni.
Alisema, kwa mujibu wa ripoti hiyo, kifo cha
Sekabenga kimetokana na mzunguko wa damu
katika mishipa kutokuwa sawa, jambo
lililosababisha ajisikie vibaya na hatimaye
kufariki dunia.



Mwili wa marehemu Sekabenga Pius
Mwakimenya ukiwa kwenye jeneza.

“Daktari amesema kwamba mishipa ya damu
haikuwa ikifanya kazi vizuri hali iliyomsababishia
ajisikie kuchoka kwa sababu damu haikuwa
ikifika sehemu zote za mwili wa marehemu,”
alisema Mwigune.
Uwazi lilifunga safari hadi chuoni na kuzungumza
na baadhi ya wanafunzi ambao walionyesha
wasiwasi kuwa huenda marehemu aliamua
kujiua kwa sumu kwa maelezo kuwa, siku
chache kabla ya kifo chake alionekana mwenye
mawazo mengi.



                   Sekabenga akiagwa.

“Hakuwa mwenye furaha, ni kama alikuwa na
jambo zito linalomsumbua ndiyo maana unasikia
wanafunzi wengi hapa chuoni wanahusisha kifo
chake na sumu,” alisema denti mmoja kwa sharti
la kutotajwa jina lake.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa familia
inayonukuu ripoti ya daktari inaziba minong’ono
yote kwa kuwa haionyeshi mahali popote kuwa
marehemu alijiua kwa sumu.



Mwili wa Sekabenga ukiingizwa kwenye gari.

Marehemu Sekabenga alikuwa mwaka wa pili
chuoni hapo akichukua Shahada ya Kwanza ya
Biashara na Uhasibu, mwili wake umesafirishwa
Jumamosi Mei 31, mwaka huu kwenda mkoani
Mbeya kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika jana
Jumatatu.

No comments:

Post a Comment