Imetokea kushangaza wengi sana kwa tukio hili la aina yake
alilosababisha msanii wa Bongo fleva mwenye miondoko tofauti kabisa na
ya HipHop, Story nzima ilikuwa hivi: Wakati mzee wa mitulinga maarufu
kama Prof J alipokuwa anaperform huko mjini Songea kwenye Kili tour,
mara ghafla shilole akavamia shoo na kuanza kuimba Nyimbo ya zali la
mentali, aliyokuwa anaiimba Professor J, jambo hili lilisababisha
mashabiki wengi sana kupiga kelele za shangwe pale kati wakimshangilia
mwanadada huyo na kuwaacha wengine midomo wazi wa kutoamini kwa tukio
hilo lililotokea.Hii inaonyesha kukubalika sana kwa mkongwe huyu hata na
wasanii wenzake, na wengine kushindwa kujizuia kupiga shangwe hasa pale
akikumbushia nyimbo zake zilizowahi ku-make headlines enzi za mwalimu.
No comments:
Post a Comment