Pages

Pages

Pages

Friday, 23 May 2014

TICHA AVUNJA NDOA YA MTU......(MICHEPUKO SIO DILI).

RB namba STK//RB/4457/2014 -KUTUMIA
LUGHA YA MATUSI inawahusu wanandoa
waliodumu kwa zaidi ya miaka 10, waliofunga
ndoa kwa mbwembwe nyingi, Nyange na Ruth
kisa kikielezwa kuwa ni ticha anayedaiwa
kuvunja utatu huo mtakatifu, Ijumaa lina kisa
na mkasa.



Ruth na Nyange wakati wa harusi.


Habari zilieleza kwamba wahusika ni wakazi wa
Pugu, Dar.
Kwa mujibu wa habari za mtaani wanakoishi
wawili hao wanadaiwa kufikishana kwenye Kituo
cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar baada ya mke
kumfungulia mumewe jalada hilo la kesi baada
ya ndoa yao kupigwa kimbunga.
Kuna madai mazito kwamba mke anamlalamikia
mumewe kumjali zaidi hawara ambaye anadaiwa
naye ni mke wa mtu akiwa ni mtumishi wa
serikali yaani mwalimu.
Akisimulia kila kitu kwa gazeti hili, Ruth
aliyefukuzwa na mumewe alisema kwamba utatu
wake na mumewe uliingia mchanga kitambo
bila yeye kujua chanzo kwani hakuwa mfuatiliaji
lakini baada ya kufuatilia alibaini kuwa kuna
mchepuko kwenye ndoa yake.



Ruth na Nyange wakiwa wenye furaha wakati wa
ndoa yao.



“Nilikuwa sijui ndoa yangu inachezewa na mtu
gani, baadaye nilinasa mawasiliano ya simu
ilibidi nifanye uchunguzi wa kina ili kumbaini
mbaya wangu kitu ambacho nilikifanikisha kwa
kiasi kikubwa alisema Ruth.
Kutokana na hali hiyo mume wake aliendelea
kufanya manyanyaso huku akiendelea na
mawasilino ya karibu na mwalimu huyo ambaye
pia ni mke wa mtu.
Mama huyo alidai kuwa mume wake amekuwa
na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mtu
huyo ambaye ni huyo mwalimu na kusababisha
pia ndoa yake kuingia matatani.
Ninachokizungumza ni sahihi kwa sababu hata
siku ninamkamata mume wangu alikuwa kwa
mwalimu huyo ambapo siku hiyo alimpelekea
sukari na matumizi mengine hali iliyosababisha
timbwili kubwa, nilifanikiwa kumnyang’anya
mume wangu ile mizigo aliyokuwa amepeleka
kwa huyo mwanamke.
Mpaka sasa tunavyoongea huyo mwalimu ndoa
yake iko matatani kutokana na jeuri aliyokuwa
akipewa na mume wangu maana inadaiwa kuwa
hata nyumba anayoishi mume wangu ndiye
mlipa kodi.
Katika kikao kilichokaa shuleni mwaka jana
kwa mwalimu huyo kuhusiana na tukio hilo,
mwalimu huyo alikiri kuwa na mahusiano na
mume wangu lakini aliahidi kuachana naye
mbele ya kikao hicho, cha kushangaza hadi leo
bado wanaendelea na mahusiano.
Alipoulizwa mwalimu huyo ambaye ametajwa
kwa jina moja la Catherine Rokio Mayengo au
Elizabeth Rokio Mayengo kwa njia ya simu
kuhusiana na sakata hilo alimwambia
mwandishi wetu kuwa namuuliza kama nani.
Mwandishi alijitambulisha na kumwambia
anataka kujua hayo yanayosemwa na Ruth
Nyange mwalimu yana ukweli gani.
Mwalimu huyo alisema hawezi kuongea na
udaku hivyo kama ni kuandikwa habari hiyo
iandikwa kadiri mwandishi anavyoweza.
Mbali na hilo mwalimu huyo alimwandikia
ujumbe mwandishi wetu unaosema kuwa yeye
anamilikiwa na serikali na haogopi kitu au
jambo lolote na anajiamini na anapenda watu
wanaotumwa kama mwandishi waende
Stakishari.
Mwandishi wetu alifanikiwa kumpata mume wa
mwalimu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina
la Evansi na kukiri kuwa huyo ni mke wake wa
ndoa lakini hawako naye kwa muda huu.
Kuhusu mke wake kuwa na uhusiano na mtu
mwingie, alisema inawezekana maana alianza
ukorofi na kuamua kwenda kupanga lakini
taarifa zilizopo amepangishiwa na mwanaume
ambaye yeye hamjui.
Huyo mwalimu ni mke wangu wa ndoa hata
mimi ninashangaa kuacha ndoa yake na kwenda
kupanga na kuacha watoto wawili ambao
tumezaa wote wakiwa wanateseka kwa kukosa
mapenzi ya mama.
Mwandishi wa habari hii alifanya kila mbinu ya
kukutana na mlalamikiwa ambaye ni Grey
Godwin Nyange lakini ilishindikana na kujibu
kwa njia ya simu kuwa habari anazoambiwa
hazifahamu labda huyo aliysema hayo ndiye
anayejua undani wake.

No comments:

Post a Comment