Pages

Pages

Pages

Wednesday, 28 May 2014

PICHAZ......WAPAMBE WA HARUSI WAMFATA WODINI VICKY KAMATA.



MAMBO yanazidi kuwa mambo kuhusu ile ndoa
ya Mbunge Vicky Kamata iliyoyeyuka katika
dakika za majeruhi, safari hii Risasi
Mchanganyiko limefanikiwa kuwanasa baadhi ya
wapambe ambao walitakiwa kuwa kwenye
msafara wa harusi hiyo kutoka kanisani hadi
ukumbini.


Baadhi ya wapambe waliotakiwa kuwepo katika
harusi ya Vicky Kamata walipomtembelea
wodini
Wapambe hao walitia timu kwenye wodi
aliyokuwa amelazwa Vicky katika Hospitali ya
General iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam,
Jumamosi iliyopita (ambayo ndiyo ilikuwa ndoa
ifungwe).

WAPAMBE WATATU
Katika idadi ya watu sita waliofika kumjulia hali
Vicky, watatu wakiwemo wanaume wawili ndiyo
waliokuwa wamevaa sare ya harusi hiyo ambayo
ingetawaliwa na rangi ya purple ‘papo’ (angalia
picha ukurasa wa mbele).

SARE KAMILI
Iilithibitika kwamba sare za shughuli hiyo
zilishashonwa, wanaume waliokuwa mstari wa
kusindikiza maharusi walitakiwa kuvaa suti
nyeusi (single button), shati jeupe na tai fupi
(necktie) yenye rangi ya papo.


Wapambe wakiwa wodini kumfariji Vicky.


Kwa mujibu wa chanzo chetu, wanawake ambao
pia walikuwa kwenye msafara wa maharusi (ma-
maids) walitakiwa kuvaa magauni ya rangi
hiyohiyo ya papo.

KWA NINI WALIVAA HUKU WAKIJUA HARUSI
HAIPO?
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wapambe hao
walikuwa ndani ya mavazi hayo kwa sababu
walijua baada ya ndoa kuyeyuka, wasingeweza
kuvaa siku nyingine.
“Unajua wale si kwamba walikwenda pale na
sare wakijua ndoa ipo, walijua kabisa kwamba
haipo ila sasa kwa sababu ndiyo ilikuwa siku
yenyewe ilibidi wajipigilie tu kama kusafisha hali
ya hewa au wengine husema ‘kuoshea’ jina,”
kilisema chanzo.


                      Vicky hospitalini.

UKUMBI WADODA
Waandishi wetu Jumapili iliyopita walikwenda
mbele zaidi kwa kufika kwenye Hoteli ya Hyatt
Regency The Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam
ambako shughuli ya ndoa hiyo ingefanyikia.
Mfanyakazi mmoja ambaye aligoma kutaja jina
kwa sababu si msemaji wa hoteli hiyo alisema
ukumbi ambao ulikuwa utumike kwa harusi ya
Vicky Kamata uitwao Kili Marquee ulilala doro
baada ya wahusika kuweka wazi kwamba
hakuna harusi tena.


...Akifarijiwa.

“Ukumbi ulilala mtupu, taarifa zilishakuja
mapema kwamba hakuna harusi,” alisema
mfanyakazi huyo.
Alipoulizwa ni kwa nini wasikodishe kwa mtu
mwingine, mfanyakazi huyo alisema si utaratibu
wa hoteli hiyo.
“Wale walishalipia, sasa ukisema ukodishe kwa
wengine kwa sababu harusi haipo, je, ingetokea
harusi ikaja ghafla na kukuta wateja wengine? Si
ingekula kwetu?” Alisema mfanyakazi huyo.

MILIONI 40 ZA MCHANGO ZATATIZA
Kuna habari kwamba, zaidi ya shilingi milioni
arobaini ambazo zilikuwa za mchango wa harusi
hiyo zimetoweka kusikojulikana.
Fedha hizo zilichangwa na wadau mbalimbali
katika kufikia kile kiasi cha shilingi milioni 96
ambazo zilidaiwa tangu awali kwamba ndizo
zingefanikisha shughuli nzima ya harusi hiyo
iliyotarajiwa kuwa ya kifahari.


Vicky Kamata akiwa katika pozi na mwanaume
aliyepanga kuoana naye anayejulikana kwa jina
la Charles ambaye kwa sasa hajulikani alipo.


BWANA HARUSI HAJULIKANI ALIPO
Ili kupata uwiano sawa wa habari hii, juzi
Jumatatu waandishi wetu walimtafuta
mwanaume aliyetarajiwa kufunga ndoa na Vicky,
Charles kwenye ofisi ya kampuni moja ya simu
za mkononi, Kijitonyama jijini Dar lakini baadhi
ya wafanyakazi walisema ana wiki mbili
hajakanyaga kazini.
“Huyu bosi hajakanyaga hapa wiki mbili,
hayupo,” alijibu mfanyakazi mmoja.
Risasi Mchanganyiko: “Hajakanyaga kivipi?
Kasafiri, yuko likizo au?”
Mfanyakazi: “Aliandika barua ya kuomba
mapumziko ya wiki mbili kwa hiyo hatujui yuko
wapi kwa sasa.”

Vicky Kamata akiendelea kupata matibabu
katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar.


NYUMBANI KWA VICKY
Baada ya kutoka ofisini kwa bwana harusi,
wanahabari wetu walitinga nyumbani kwa bibi
harusi Vicky Kamata, Sinza ya Vatican, Dar na
kukumbana na mlinzi getini ambaye alisema
mgonjwa huyo aliruhusiwa kutoka hospitali saa
mbili usiku wa Jumapili lakini alikuwa amelala
na haruhusiwi kuzungumza na mtu yeyote zaidi
ya kupumzika.
“Mheshimiwa karudi jana usiku saa mbili lakini
haruhusiwi kuzungumza na watu, amelala,”
alisema mlinzi huyo.

No comments:

Post a Comment