Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Pages
▼
Pages
▼
Pages
▼
Friday, 30 May 2014
JE MWANAMKE UNATAKA KUWA SUMAKU KWA MWANAUME ?
1. Mwanamke jipende mwenyewe
Mwanamke ni lazima ujipende na
kujiamini na ukigundua kuwa hisia
zako zaapenzi zimejikita kwa huyo
mwanaume ambaye hisia zako
zinaamini kuwa ni yule ambaye
umewahi kumuwaza kuwa ungependa
kuwa nae basi usieleze kwanza uongo
maana akija gundua weeeeee……noma.
Hapa niweke wazi kuwa ni muhimu
mwanamke au mwanaume,
kwa pamoja tujue kuwa tofauti yetu na
mbuzi siyo miguu au
manyoya bali kitu kingine kikubwa
zaidi. Kitu hikikikubwa
ndicho sisi – sisi ni jinsi tunavyofikiri
ambapo kwa kufikiri
kwetu tunakuwa kama tulivyo ambao
ndiyo sisi wenyewe.
2. Jifunze namna ya kuzuga
Sisemi jifunze namna ya kudanganya
bali ‘’kuzuga’’ naamini naeleweka
vema ambapo wanawake wengi wenye
kujua kuzuga wamekwa sumaku
kubwa kwa wapenzi wao ama kwa
wabnaume wanaowahitaji.
Wanawake wenye ujuzi wa kuzuga
wamekuwa wakifanikiwa kuwanasa
wanaume wengi kutokana na ujuzi wa
kutumia viungo vyao walivyop
[ewa na Mungu huku baadhi wakitumia
macho yao kwa kuangaliana
mara kwa mara na wanaume
wanaovutiwa huku baadhi wakitumia
midomo yao kuilamba kana kwamba
anasawazisha mafuta katika
midomo hiyo.
Mbinu hii inawapagawisha wanaume
wengi ambao hujikuta akikuuluza
jina ama moja kwa moja akakusogelea
na kukusabahi na kujitambulisha
ama kuomba namba yako ya simu, si
unajua utandawazi umewapotezea
wanaume wengi ujasiri wa kutongoza
zaidi atakupigia simu, si mnajua
wengi tunatongozana kupitia simu…si
vibaya ingawa hamu inapotea kidogo.
3. Panga ratiba ya kutoka, ‘’siyo
kusaka mabuzi’’
Wanawake wengine wamekuwa
wakilaumu kuwa hawatongozwi na
wanashindwa kuwadaka wanaume
wanaowataka kimapenzi huku
wao wenyewe wakiwa tatizo. Wengi
hushinda nyumbani kama
watoto wa Mfalme jambo ambalo
wengine wamejikuta
wakizeeka na kuanza kukumbuka hata
kwa kulazimisha
kuwa walau nwapate watoto.
Hali hii mwanamke utaiepuka endapo
utakuwa na walau na
ratiba zako nzuri hata kama haupendi
kwenda Disko au ni geti kali basi hata
week end uwe na ratiba ya kutembea
ufukweni au mahala ambako unajua
kuna
watu wanajichanganya kidogo majira
ya jioni na ahapa sizungumzii kuwa
unaenda kutafuta soko bali kama
unajiamini kuwa unamvuto naamini
uchaguzi
wako utakuwa mgumu kwasababau
wengi watatamani kuwa nawe, si
unaushawishi banaaaa…
4. Kosoa kwa hekima
Mbinu hii itawasaidia sana wanawake
ambao wapo tayari kwenye ndoa
na mahusiano ya kawaida ambapo
kuna mahala wanawake wanajisahau
na
kuwatamkia wanaume wao maneno
yasiyo na hekima, kwa mfano utamsikia
mwanamke anamwambia mwanaume
wake kuwa ‘’wanaume wenzako
wanajenga, wewe kila siku ahadi tu’’
kauli kama hii ni kosa na kasoro
kubwa.
Ukiachiliambali kwamba hiyo ni
lawama, lakini kauli kama hiyo
inajenga
hisia kwa mwenzako kuwa mwanamke
huyu kumbe anapenda kuwa
na wanaume kama hao hivyo wanaume
wengi hawapendi kushauriwa
bila hekima na kudhani kuwa
wanawake hao wanaodhani wanaume
wao hao siyo wa maana hivyo
mwanamke ukitumia maneno yasiyo
na hekima huwezi kuwa sumaku kwa
mwanamume wako.
Kwa leo tuishie hapa wiki ijayo na
kuendelea nitakuletea mfululizo
wa tofauti zetu yaani mwanamke na
mwanaume na ujua kuwa
kutentewa vizuri na mpenzi wako ni
haki yako au la na hapo tutaelezana
madogomadogo yafukuzayo wapenzi.
No comments:
Post a Comment