Pages

Pages

Pages

Sunday, 25 May 2014

BIBI WA MIAKA 65 AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE(PICHA).


Mama huyu ashangaza watu baada ya kubeba kete 20 kwa wakati mmoja.


Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole
(65) amevunja rekodi ya umri wa watu
wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA). Cole alikamatwa Jumatatu
akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini
zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi
zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si
rahisi kuonekana katika mitambo. Habari
zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa
Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya,
Alfred Nzowa zimesema pamoja na mbinu zake
na kujiamini, mwanamke huyo alikamatwa
kutokana na ushirikiano wa vitengo mbalimbali
vya uwanja wa ndege.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege,
Hamisi Selemani alisema mwanamke huyo
alikamatwa Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri
akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya
Shirika la Ndege la Ethiopia.
Selemani alisema raia huyo aliwasili nchini Mei
15, mwaka huu na alikaa muda wote bila ya
kuwa na shughuli yoyote, jambo ambalo lilitiliwa
shaka na kumkamata.
“Huyu mwanamke achana naye, akisimama
mbele yako huwezi ukaamini kwa jinsi
anavyojiamini. Alikuwa na mbinu mpya ya
kufunga hizo kete. Kila moja ilifungwa kwa
karatasi inayofanana na ganda la sigara,”
alisema Selemani.
Alisema mwanamke huyo alitumia mbinu hiyo ili
asigundulike wakati akikaguliwa kwa mitambo
maalumu inayogundua dawa za kulevya.
Taarifa zaidi zinasema kuwa kutokana na mbinu
yake ya ufungaji wa kete, mwanamke huyo
alikuwa tayari amevuka hatua ya kwanza ya
ukaguzi.
Nzowa alisema baada ya kumhoji, mtuhumiwa
huyo alidai kuwa aliingia nchini kwa ajili ya
kutafuta soko la kuuza vipodozi na nguo.
“Wakati tukiendelea kumhoji, Kikosi Kazi cha
Kuthibiti Dawa za Kulevya kilibaini na kugundua
kuwa alikuwa amemeza dawa za kulevya.
“Huyu ni mzee, lakini tumeshangaa kuona bado
ana nguvu za kutosha na tulishangaa baada ya
kutoa kete 20 kwa mara moja katika awamu ya
kwanza, jambo hili si rahisi kutokana na umri
wake,” alisema Nzowa.
Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na hati ya kusafiria
ya Nigeria, anaendelea kuhojiwa na upelelezi
ukikamilika atafikishwa mahakamani

No comments:

Post a Comment