Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua
wasanii Jakob Steven Jb na Steve Magele
Nyerere wamepiga nguvu kavukavu karibu na
eneo la msiba wa marehemu Adam Kuambiana
huko Bunju huku kisa kikiwa kugeukana kwenye
dili la matangazo.
Habari za uhakika zilizotua mezani kwa
Maskanibongotz zilisema kuwa msanii steve
nyerere ndiye aliyeanza kumchokoza msanii Jb
kwa kumchana baada ya kumgeuka kwenye
mchongo wa matangazo ya kampuni moja ya
simu iliyopo maeneo ya Moroco Jijini Dar.
Habari zaidi zilisema wakati wasanii hao wakiwa
baa wanakula kijala siku moja kabla ya mazishi
ya msanii mwenzao Steve alimvamia Jb na
kuanza kumchana na kumueleza jinsi alivyokuwa
na roho mbaya kwa kumgeuka kwenye mchongo
wa mtangazo ya simu pale Moroco na kusema
ndiyo maana anaroho mbaya.
Majibizano hayo yalidumu kwa muda mrefu sana
huku Jb akiwa kimya kwani stevu alionekana
kuumizwa na jambo hilo kwani inadaiwa zile
picha za Jb kwenye mabango ya mtandao huo
wa simu mchongo alipewa na steve lakini
baadae Jb alimgeuka na kwenda kupiga
mchongo kimaya kimya na kumuacha Steve
akishangaa.
Hata hivyo Steve aliendelea kusasambua Jb
mbele ya watu hali hiyo ilimfanya Jb kunyanyuka
na kuanza kufokea nae huku akimtahadharisha
kama atamfinyangafinya na ufupi wake ndipo
steve nyerere aliyekuwa ameshika chupa ya kilaji
aliruka kichwa kimoja kilichompiga Jb kifuani na
kupepesuka.
Wakati watu akijianda kwenda kuamulia basi
Steve ambae aliwahi kucheza ngumi miaka ya
nyuma alimshindilia Jb ngumi kama tisa za
harakaharaka sehemu ya tumbo iliyomfanya Jb
kudondoka chini na kushindwa kupumua kwa
dakika tano kisha alinyanyuka na kukalia kiti.
Maskanibongtz iliwasiliana na wasanii hao ili
kupata ukweli wa mambo lakini kwa bahati
mbaya simu zao hazikupekelewa na bado
tunawatafuta.
CREDIT:MaskaniTz.
No comments:
Post a Comment